Wanawake wa Imani
Wanawake wa Imani
Soma Biblia
Vipindi vya wanawake wa Kikristo. Masungumso kuhusu mambo ya maisha. Vipindi vyote ni Kiswahili.
Kupendwa na Mungu - Wanawake wa Imani Kip #1
Je, umezingatia kwamba sisi wanawake tunacho kitu kama sanduku mioyoni mwetu. Sehemu inayopaswa kujaa upendo. Ni jinsi Mungu alivyotuumba. Lakini mara nyingi ninasikia utupu hapo, au tuseme nina kiu. Kiu ya kupendwa. Ebu fikiria ungeambiwa maneno matamu haya: “mna thamani mbele yangu, kwa kuwa nimewapa hadhi na kuwapenda.” Haya ni maneno ya Mungu.
Jul 2, 2018
31 min
Anakupenda kwa sababu alikuumba - Wanawake wa Imani Kip #2
Tunafahamu kwamba tuna shida mbalimbali katika maisha yetu. Shida ya uchumi ni rahisi kutambua, na wengi wanapambana kila siku ili wapate hata kidogo tu cha kulisha familia. Kwa nini Mungu haoni hali hii na kunisaidia kama ananipenda?
Jul 1, 2018
32 min
Yesu anapiga hodi kwako - Wanawake wa Imani Kip. #3
Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. Uf. 3:20
Jun 30, 2018
33 min
Mwanamke Msamaria anawekwa huru na Yesu
Mwanamke tutakayemkuta leo alikuwa anatafuta upendo, uhuru na amani kama tulivyoongea kipindi kingine, sisi wote tunatafuta mambo haya juu ya mambo yote mengine. Lakini huyu mwanamke pale alipoangalia na kutafuta, hakuweza kuyapata. Labda pia wewe uko kwenye hali ya kutafuta sana upendo, uhuru na amani, lakini baado hujayapata vizuri. Labda unaangalia mahali ambapo haipo!
Jun 29, 2018
38 min
Ushuhuda wa Dorena Jakobo 1/2 - Wanawake wa Imani kip. #5
Mama Neema anaongea na Dorena Jakobo aliyekutana na vikwazo vingi maishani mwake.
Jun 28, 2018
26 min
Ushuhuda wa Dorena Jakobo 2/2 - Wanawake wa Imani
Mama Neema anaongea na Dorena Jakobo, "Mama Eliyah", kuhusu jinsi baba yake Dorena, aliokoka kupitia yeye.
Jun 27, 2018
25 min