
Kuna surprise kibao kwenye Ligi Kuu Tanzania bara ambazo tumeziona baada ya Game week mbili.
Matumizi ya washambuliaji wawili
Timu kuhamia back-four
Mawinga wenye speed
Singida Big Star
Aziz Ki vs Chama
Sikiliza episode hii kuyajua yote hayo kisha tupe maoni yako
Aug 31, 2022
28 min

Tangu amechukua mikoba ya kukinoa kikosi cha Chelsea, Tuchel amekuwa akihusudu mfumo wa mabeki watatu kuliko ule wa mabaki wanne ambao alikuwa akiutumia akiwa PSG.
Clifford Sangai na Prosper Bartalomew wanajadili kwa kina falsafa za raia huyo wa Ujerumani. Miongoni mwa yaliyoongelewa ni kama Tuchel anaweza badili mfumo au atasalia na wa sasa? Kitendawili cha Havertz, Werner na Lukaku bila kusahau namna anavyotegemea Wingback wakati wa kufanya mashambulizi.
Sikiliza zaidi Episode hii
Jun 3, 2022
23 min

Ni mwaka mmoja sasa tangu Nasreddine Nabi achukue mikoba ya kukinoa kikosi cha Yanga kutoka kwa Cedric Kaze ambaye kwa sasa ni msaidizi wake.
Kuna mambo mengi ameyabadili katika kikosi hicho ambayo Clifford Sangai na Prosper Bartalomew wanayajadili katika episode hii.
Kati ya hayo ni kumfanya kiungo Feisal Salum kucheza katika eneo la mbele zaidi kuliko alipokuwa akicheza hapo awali.
Swala la muhimu zaidi ni nafasi ambayo wachezaji vijana waliopo Yanga wanapewa nafasi na Nabi.
Sikiliza episode hii kisha tupe maoni yako.
May 6, 2022
24 min

Stars ya Kim ni tofauti na ya Etienne lakini kuna vitu vinaendana. Episode hii emejikita katika kuangazia falsafa za kocha Kim Poulsen anayekinoa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'
Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili hayo yote bila kusahau aina ya wachezaji ambao Kim hapendi kuwakosa kwenye timu. Je ni wachezaji gani hao? Sikiliza Episode hii hadi mwisho
Apr 6, 2022
16 min

Tangu miaka ya 90 wapenzi wa soka walianza kushuhudia kazi za Carlo Ancelotti ambaye ni raia wa Italia. Katika miaka yake yote kama kocha ameshuhudia mabadiliko mbalimbali katika soka barani Ulaya lakini amwezaje kudumu katika taaluma hiyo kwa kipindi kirefu?
Clifford Sangai na Prosper Bartalomew wanajadiliana kuhusu falsafa, mbinu na ufundi wa kocha huyo ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Real Madrid kwa muhula wa pili.
Kuna mengi sana tusiyoyajua kuhusu Ancelotti, sikiliza episode hii kisha utupe maoni yako.
Mar 22, 2022
15 min

Wengi huvutiwa na soka la timu anazofundisha kama Marseille, Lille na Leeds ambayo kwa sasa imemtimua. Kuna mengi ya kujifunza juu ya falsafa ya Marcelo Bielsa na hapo ndipo kunamfanya Clifford Sangai aketi chini na Prosper Bartalomew kujadili kwa kina mbinu na ufundi wa raia huyo wa Argentina.
Tumeongelea aina yake ya ukabaji ambayo ni 'MAN TO MAN" tukiangazia kwa kina namna ilivyofaulu na kufeli hasa akiwa na Leeds United.
Prosper alienda mbali zaidi kwa kulinganisha mbinu za Bielsa dhidi ya Gian Piero Gasperini ambaye anakinioa kikosi cha Atalanta kinachoshiriki ligi kuu ya nchini Italia maarufu kama Serie A.
Sikiliza uchambuzi huu pia share na wengine zaidi.
Mar 8, 2022
15 min

Tangu Lukaku afanye mahojiano na Sky sports, amecheza mechi sita za Ligi Kuu bila kufunga bao. Clifford Sangai ameamua kukaa chini na Prosper Bartalomew kuangalia mwenendo wa mshambuliaji huyo wa Chelsea ambaye msimu uliopita alifunga mabao 24 na assists 11 akiwa na klabu ya Inter. Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni mifumo ya Chelsea, Inter Milan na timu ya taifa ya Ubelgiji. Prosper ameenda mbali zaidi kwa kuangalia aina ya pasi ambazo Lukaku anapokea pia maeneo anayokaa ili kupokea pasi. Episode hii imeelezea kila kitu kuhusu Romelu Lukaku.
Feb 22, 2022
13 min

Bila shaka ulimsikia beki wa Mtibwa Sugar, Abdi Banda aliposema kwamba washambuliaji wa Simba ni rahisi kuwakaba. Je kauli hii inaukweli?
Clifford Sangai amekutana na Prosper Bartalomew chini ya mti ili kuangazia na kuchambua kwa undani mikimbio ya washambuliaji wa Simba yaani Kagere, Mugalu na Bocco
Usisite kushea na marafiki Episode hii
Pia unaweza kupakua majarida yetu BURE kuhusu AFCON:
https://sportscasttz.gumroad.com/l/stajt
https://sportscasttz.gumroad.com/l/jbxud
Feb 1, 2022
16 min

Hawakuanza msimu vizuri lakini hivi karibuni inaonekana kama gari limewaka.
Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia wapi Arsenal walikuwa wanakwama pamoja na vitu ambavyo Mikel Arteta ameviongeza ili kuongeza ubora katika safu ya ushambuliaji.
Tumegusia pia patnership ya Xhaka na Partey inavyowasaidia katika kufanya mashambulizi.
Katika episode hii tumegusia mbinu za Mikel Arteta kwa undani zaidi, usisite kuisikiliza hadi mwisho.
Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
Jan 11, 2022
19 min

Watani hawa wa jadi wametuonesha mambo mengi katika mechi mbili walizokutana, kuanzia maswala ya ufundi hadi mbinu za makocha wao na hapo ndipo Clifford Sangai anapojadiliana na Prosper Bartalomew kuhusu timu hizo.
Tumeangazia eneo moja muhimu sana kwa timu zote mbili nalo ni Safu ya Viungo ambapo kila timu imeonesha ubora na madhaifu yake na kama yanaweza kusahihishwa.
Unataka kujua madhaifu hayo basi sikiliza episode hii
Dec 14, 2021
21 min
Load more
