Meza Huru
Meza Huru
Meza Huru
Tanzanian music, from Genesis to currently status told by Stake holders.
Mezani na MANDOJO NA DOMOKAYA #18
Usichofahamu ni majina yao halisi Joseph Francis Michael Ong'oso na Precious Juma Mkoma maarufu kama Man'Dojo na Domokaya. Wanamuziki mashuhuri sana wa kizazi cha jana na leo.  nani asiyepende kusikia sauti nzuri na za kuvutia zikisindikizwa na Guitar lao(wenyewe wanaliita Banjo)?  Nani asiyetambua uwezo wa miamba hawa wa muziki katika kuweka viitikio na vionjo makini katika nyimbo mbalimbali za Muziki wa Kibongo? Hawa ni marafiki waliogeuka ndugu, wenyewe wanadai wamepitia mpaka kuvaa nguo sare 😁 Meza Huru imekaa nao na kupata simulizi ya maisha yao ya muziki na amini kwamba, inavutia sana.  Jumuika nasi mezani kuwasililiza 😊, Karibu  #MezaniNaMandojoNaDomokaya  #MezaHuru
Nov 25, 2022
2 hr 30 min
Mezani na KIBACHA Part II
Sehemu ya pili ya maongezi yetu na KBC, ambaye wengi wanamfahamu kama Kibacha Huyu ni mojawapo wa mwamba muhimu wa Hip Hop ya Tanzania. Unaambiwa zama zake, Kipaza kilimuogopa kama ukoma, Rafiki wa mashairi na mchenguaji mashuhuri. Gwiji wa mtindo huru na Battle Emcee haswaaa.  Kibacha ni miongoni mwa waanzilishi wa Kundi kongwe na mahiri la KWANZA UNIT. Ametupa heshima kubwa ya kukaa nasi na kutupa historia ya muziki wake tangu miaka ya 80 mpaka hapa tulipo. Mwamba huyu hapa 😊 #MezaniNaKBC  #MezaHuru 
Nov 22, 2022
1 hr 41 min
Mezani na KIBACHA Part I
Anaitwa KBC, wengi wanamfahamu kama Kibacha Huyu ni mojawapo wa mwamba muhimu wa Hip Hop ya Tanzania. Unaambiwa zama zake, Kipaza kilimuogopa kama ukoma, Rafiki wa mashairi na mchenguaji mashuhuri. Gwiji wa mtindo huru na Battle Emcee haswaaa.  Kibacha ni miongoni mwa waanzilishi wa Kundi kongwe na mahiri la KWANZA UNIT. Ametupa heshima kubwa ya kukaa nasi na kutupa historia ya muziki wake tangu miaka ya 80 mpaka hapa tulipo. Jumuika nasi mezani kumsikiliza Mwamba huyu hapa 😊 #MezaniNaKBC  #MezaHuru 
Nov 18, 2022
1 hr 39 min
Mezani na DOLO #15
Anaitwa DOLOMOI FRANCIS, kwa jina maarufu anafahamika kama DOLO. Ni moja ya waasisi wa kundi la Wachuja Nafaka na Wanaume TMK.  Kutoka maeneo ya TEMEKE.  Tumepata bahati ya kukaa naye mezani na ametupitisha kwenye safari yake ya muziki. Kuanzia akiwa hajawa Dolo,  mpaka hivi sasa akiwa bado anapeperusha vyema bendera ya TMK. #MezaniNaDolo  #MezaHuru
Nov 11, 2022
2 hr 9 min
Mezani na KR MULLAH #14
KR Mullah ,miongoni mwa waasisi wa GWM (Gangstaz With Matatizo), Wachuja Nafaka, TMK Wanaume family Mwamba huyu kutokea Temeke Dar es Salaam amefanya makubwa sana katika muziki wetu kabla haujaanza kuwa rasmi Amefanya kazi na wakongwe kama Boniluv, Master Jay na P Funk. Ametupatia heshima kubwa ya kutupa simulizi yake tangu akiwa kijana mdogo katika muziki mpaka sasa bado anawakilisha Temeke popote pale alipo Muite KR Mullah Jibaba Muziki Mkubwa CD Mia Saba Njoo kichwa kichwa akupe za uso saba. #MezaniNaKakaRashidi  #MezaHuru
Nov 4, 2022
1 hr 30 min
Mezani na RAS INNO #13
Ras Innocent Nganyagwa ni miongoni mwa wanamuziki nguli katika kizazi cha tatu cha muziki wa Reggae kutoka Tanzania.  Muziki wa Reggae Afrika ulianza kushamiri baada ya Uhuru wa Zimbabwe mwaka 1980, Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizokuwa za mwanzo kupata mapokeo ya muziki huo. Tumezungumza na Ras Inno kuhusu imani ya RastaFari, muziki wa Reggae Ras Innocent Richard Nganyagwa ni shule haswa, Ana ufahamu mkubwa sana wa maisha ya asili ya mwafrika na anaamini kila mtu mweusi ni Rastafarian. Ras Inno ni mtetezi wa haki za binadamu na za wasanii pia, Jumuika nasi mezani umsikilize, Karibu. #MezaniNaRasInno  #MezaHuru  Anchor - https://anchor.fm/meza-huru Google podcast -  https://podcasts.google.com/feed/aHR0...  Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683 Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r...  Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797 Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2...  Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087 Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru...  YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...    Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10...  Twitter - https://twitter.com/MezaHuru
Oct 28, 2022
2 hr 6 min
Mezani na CAROLA KINASHA #12
Carola Kinasha, ukimuona huwezi kuamini ana miongo sita duniani. First lady wa Bene Bene na baadaye Shada. Msomi wa chuo kikuu aliyechagua kufanya muziki kama kazi. Mwanaharakati wa mwanzo kabisa wa stahiki na haki za utunzi, na moja walioupeleka mbali sana muziki wa asili ya Afrika. Ni mcheshi na mwenye maarifa mengi sana kuhusu maisha na safari ya muziki wetu tangu miaka ya themanini mpaka leo hii. Unajua kisa chake na Remmy Ongala kilichozaa kibao maarufu cha Karola? Unajua nini maana ya segese? Unajua kwamba yeye ni mtu aliyekuwa nyuma ya chorus nzuri na tamu za Bongofleva yetu hii? Carola Kinasha ni nyota wa muziki wetu na Almasi inayowaka kama taa.  Jumuika nasi mezani umsikilize, Karibu #MezaniNaCarolaKinasha  #MezaHuru  Anchor - https://anchor.fm/meza-huru Google podcast -  https://podcasts.google.com/feed/aHR0...  Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683 Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r...  Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797 Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2...  Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087 Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru...  YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...    Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10...  Twitter - https://twitter.com/MezaHuru
Oct 21, 2022
2 hr 17 min
Mezani na MIKE TEE #11
Wengi wanamjua kwa jina la Mnyalu, Mike Tee, The Dangerous Emcee ila jina lake kamili ni Mike Francis Mwakatundu.  Mike Tee alianza kuimba mwanzoni mwa miaka ya 90, akiimba kwaya kanisani na taratibu akaanza kujifunza kuandika na kuimba mistari kupitia mashairi ya gazetini baada ya kukutana na Ntwa mmoja wa waanzilishi wa WWA (Wagumu Weusi Asilia). Amefanya kazi na watayarishaji kama P Funk na Master Jay, amefanya hits na wasanii kama Juma Nature, Q Chief, Mad Ice na Komando Jide Unajua kuhusu ugomvi wa Mr. Nice na Dudu Baya? Mike Tee amenyoosha taarifa. Sitaki kumalizia stori yake. Jumuika nasi mezani umsikilize, Karibu #MezaniNaMikeTee  #MezaHuru  Anchor - https://anchor.fm/meza-huru Google podcast -  https://podcasts.google.com/feed/aHR0...  Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683 Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r...  Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797 Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2...  Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087 Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru...  YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...    Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10...  Twitter - https://twitter.com/MezaHuru
Oct 14, 2022
1 hr 58 min
Mezani na UNCLE JOHN KITIME #10
Mzee Kitime ama Ango "Uncle" Kitime kama mwenyewe anavyojitanabaisha kwenye mitandao. Ni mwanamuziki nguli wa Muziki wa Dansi kutoka Kilimanjaro Band maarufu kama "Wana Njenje", mmoja wa wanakamati ya kutetea muziki wa dansi na tasnia ya muziki kwa ujumla, Mtangazaji wa Radio, Muigizaji wa Filamu, Mchekeshaji na Mtunza historia ya Music wa Tanzania. Tumekaa naye na kupata historia ya muziki wake na harakati zake tangu mwaka 1967 hadi leo akiwa na JFK BAND. Jumuika nasi mezani tumsikilize Gwiji huyu wa Tasnia yetu, Karibu. #MezaniNaJOHNKITIME  #MezaHuru  Anchor - https://anchor.fm/meza-huru Google podcast -  https://podcasts.google.com/feed/aHR0...  Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683 Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r...  Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797 Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2...  Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087 Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru...  YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...    Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10...  Twitter - https://twitter.com/MezaHuru Instagram - https://instagram/mezahurupodcast
Oct 7, 2022
2 hr 17 min
Mezani na MASTER JAY Part II
Sehemu ya pili ya maongezi na Master Jay. Kama hujasikiliza nyimbo alizotengeneza (naamini ni vigumu), utakuwa umemuona kwenye mashindano ya kusaka vipaji Joachim Marunda Kimaryo ni Gwiji kabisa katika tasnia ya muziki wetu Amehusika katika Hip Hop, Bongofleva, Dansi mpaka nyimbo za Dini 😁 Tumepata nafasi ya kuzungumza naye na ametupa simulizi ambazo zinaweza kutumika kama chanzo rasmi cha historia za muziki wetu kuanzia mwanzo mpaka tulipo. Jumuika nasi mezani, tusikilize PART II ya MTABE huyu wa sanaa 😉 Karibu. #MezaniNaMasterJay #MezaHuru Anchor - https://anchor.fm/meza-huru Google podcast -  https://podcasts.google.com/feed/aHR0... Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683 Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r... Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797 Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2... Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087 Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru... YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp... Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10... Twitter - https://twitter.com/MezaHuru
Sep 30, 2022
58 min
Load more