
Kwenye makala haya utasikiliza uchambuzi wa mechi za kufuzu soka ya kina dada Olimpiki na shirikisho la riadha duniani kuwa shirikisho la kwanza kutoa tuzo za fedha, maandalizi kuelekea riadha za KipKeino Classic, mkusanyiko wa michezo DRC, uchambuzi wa mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Tiger Woods na Novak Djokovic waweka historia kubwa duniani kwenye gofu na tenisi mtawalia.
Apr 13, 2024
23 min

Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na uchambuzi wa hatua ya robo fainali mkondo wa pili michuano ya Klabu Bingwa Afrika, matokeo ya kufuzu soka Olimpiki ya kina dada, mwanasoka wa Afrika Kusini kuuawa, PSG Academy yatoa mafunzo kwa makocha nchini Rwanda, Kenya yatangaza orodha yake ya wanariadha wa mbio za Marathon kwenye Olimpiki ya mwaka huu, Ufaransa na Kenya kushirikiana kujenga viwanja nane nayo PSG ikiwa tayari kutoa pauni milioni 111 kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen
Apr 6, 2024
23 min

Karibu katika makala jukwaa la michezo, leo hii tumekuandalia taarifa kadhaa kuanzia katika mashindano ya mbio za magari Safari rally nchini kenya, michuano ya klabu bingwa barani afrika Al Ahly wakiishinda Simba goli moja sifuri kisha Tp Mazembe kupata sare dhidi ya Petro Atletico ya Angola na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Sierra Leone Lamin Bangura afariki akiwa na umri wa miaka 59 katika ajali ya basi.
Mar 30, 2024
23 min

Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na Kenya kuongoza chati ya medali Afrika Mashariki katika mashindano ya Afrika, Shirikisho la soka Cameroon yaondoa kashfa ya udanganyifu wa miaka dhidi ya Nathan Doualla, mkurugenzi mwandalizi wa WRC Safari Rally Jim Kahumbura ajiuzulu, droo ya soka mashindano ya Olimpiki na Nottingham Forest kupokonywa alama nne kutofuata sheria wa fedha Uingereza.
Mar 23, 2024
23 min

Karibu katika makala ya jukwaa la michezo, leo tumekuandalia mengi tukianzia na droo ya robo fainali katika michuano ya klabu bingwa barani afrika, mashindano ya bara afrika pamoja na droo ya robo fainali katika mashindano ya klabu bingwa barani ulaya.
Mar 16, 2024
23 min

Karibu katika makala ya jukwaa la michezo leo tunaangazia kushindwa kwa mwana masumbwi Francis Ngannou na Anthony Joshua,kuanza kwa mashindano ya 13 ya bara Afrika nchini Ghana pamoja na Paris Saint Germain kufuzu katika robo fainali michuano ya klabu bingwa barani ulaya.
Mar 9, 2024
24 min

Karibu katika makala ya jukwaa la michezo leo tunaangazia kujengwa kwa uwanja mpya wa michezo nchini kenya, michuano ya klabu bingwa barani afrika pamoja na taifa la ufaransa kukamilisha ujenzi wa kijiji kitakachotumiwa na wanariadha katika michezo ya olimpiki.
Mar 2, 2024
23 min

Karibu katika makala jukwaa la michezo, leo hii tunaangazia kukamilika kwa mashindano ya kuendesha baiskeli ya Tour du Rwanda, mashindano ya mchezo ya gofu Magical kenya open pamoja na klabu ya Yanga na Tp Mazembe kufuzu katika hatua ya robo fainali katika michuano ya robo fainali katika michuano ya klabu bingwa barani afrika.
Feb 25, 2024
22 min

Karibu katika makala ya Jukwaa la michezo, leo tumekuandalia mengi ikiwemo kuanza kwa mashindano ya kuendesha baiskeli ya Tour du Rwanda, mazungumzo ya kipekee na waziri wa michezo nchini Tanzania Damas Ndumbaro pamoja na kupigwa marufuku mechi nne kwa mchezaji wa timu ya taifa ya senegal Kreppin Diatta.
Feb 17, 2024
24 min

Miongoni mwa taarifa kuu tutakazozianhazia ni pamoja na fainali ya kombe la mataifa ya bara afrika AFCON kuchezwa hapo kesho mwenyeji Ivory coast wakipambana na Nigeria. Mchezaji wa tenisi nambari moja barani afrika Ons Jabeur kushindwa katika mashindano ya Abu dhabi na fainali ya kombe la mataifa ya bara Asia kuchezwa leo.
Feb 10, 2024
25 min
Load more
