H.W PODCAST - Positive Vibes!
H.W PODCAST - Positive Vibes!
Hub of Wisdom inc.
Ni muda wa kuchukua nafasi yako katika meza ya H.W nasi tutawasilisha kwako mawazo ya thamani kwa maneno ya dhahabu. Mahali pa kwanza na pekee unapohitaji kuwa kwa ajili ya ustawi wako. Karibu tujifunze vingi. Pata nafasi ya kusikiliza mambo ya msingi sana yatakayonoa stadi zako, kukuongezea maarifa na kuchochea maendeleo yako ya kiutu. #Karibu_nyumbani.
KUFIKIA KIWANGO CHA JUU ZAIDI KATIKA KILE UTAKACHOKIFANYA - Sebastian Kolowa
"Sisi sote tuna nafasi ya kustawi zaidi katika chochote tunachokifanya. Changamoto inayotukumba vijana wengi ni kwamba hatutambui na kuzifuata zile hatua muhimu zenye kutufikisha hapo. Muda ni mchache na sio sawa kwenda bila dira. Ndio maana leo nimeona niyazungumze haya yafuatayo..." Anasema Sebastian Kolowa katika mkutano wa nne wa Hub of Wisdom Community Jijini Dar Es Salaam. Fuatilia Matoleo mengine zaidi kupitia H.W TV kwa njia ya YouTube Au sikiliza kupitia H.W PODCAST. Au tuma maoni yako kwa njia ya ujumbe wa maandishi au sauti kupitia 0753825794 ili jukwaa hili lizidi kuwa bora kwa ajili yako na wengine. Tembelea www.hubofwisdom.com/media kufahamu zaidi. Tunafurahi unapojifunza lakini tunafurahi zaidi unapofanya. Nenda duniani, kafanye zaidi na uwe zaidi! --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/hubofwisdom/message
Jan 26, 2024
18 min
MAKOSA MAKUBWA YANAYOFANYIKA KATIKA MAHUSIANO NA NAMNA YA KUYAEPUKA - Sadaka Gandi #Mapenzi
"Wewe unaamini kwamba huyo mwenzako unampenda kumbe kuna makosa makubwa sana. Twende pamoja tuangalie vijana wanakosea wapi na namna gani ufanye ili kuepuka au kurekebisha makosa." Anasema Bi Sadaka Gandi, mtaalamu wa saikolojia ya familia na mshauri mbobevu katika maswala ya mahusiano. Fuatilia matoleo haya katika H.W TV kwa njia ya YouTube na kwa mfumo sauti kupitia H.W PODCAST. Pia usisite kutuandikia maoni yako ili jukwaa hili liendelee kuwa bora zaidi kwa ajili yako na wafuatiliaji wengine. Tuandikie kupitia [email protected] au tuma ujumbe wa sauti kwa njia ya WhatsApp kwenda namba 0753825794. Tembelea www.hubofwisdom.com kufahamu zaidi au tuma neno WISDOM kwenda namba 0753825794 uunganishwe katika jamii ya H.W na ushiriki vipindi hivi moja kwa moja. Endelea kujifunza, Endelea kufanya. Tunafurahi sana ukiangalia zaidi lakini tunafurahi mara dufu ukifanya. Nenda duniani ukafanye zaidi na uwe zaidi! #karibu_nyumbani Welcome to the home for positive vibes! --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/hubofwisdom/message
Jan 26, 2024
12 min
KUONGEZA THAMANI
Hauwi wa thamani kwasababu ya kile unachokipata bali kile unachokitoa. "Kwakuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna, apandaye haba atavuna haba. Apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu." Kitakachofanya bidhaa zako au huduma zako ziwe za thamani sio gharama yake bali ni manufaa yanayotokana na hiyo huduma. Ili upate faida kubwa kutokana na kile unachokifanya unatakiwa upande mbegu ya thamani. . . Fuatilia mtiririko wa matoleo haya kupitia H.W TV na H.W PODCAST kila wiki. Tembelea www.hubofwisdom.com/media kufahamu zaidi. Maoni yako ni ya thamani sana kwetu ili toleo lijalo liwe bora zaidi kwa ajili yako na wafuatiliaji wengine. Tuma ujumbe wako wa maoni kwenda namba 0753825794 au andika barua pepe kwenda [email protected] . TUNAFURAHI UKISIKILIZA LAKINI TUNAFURAHI ZAIDI UNAPOFANYA, KWAHIYO NENDA DUNIANI UKAFANYE ZAIDI NA KUWA ZAIDI! #karibu_nyumbani --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/hubofwisdom/message
Dec 11, 2023
9 min
NAMNA SAHIHI YA KUJENGA
"Start Small think Big". Zingatia mambo madogo. "Start Small, Think Big". Ukifanya vizuri katika uwanda mdogo hata siku ukiwa katika uwanda mkubwa, uwezekano ni kwamba utafanya vizuri. Wakati unapofikiria kujenga mambo makubwa anza kidogokidogo. ....................................................................... Maoni yako ni muhimu na atunayathamini sana, hivyo tuma ujumbe wako wa sauti kwa njia ya WhatsApp nasi tutaumbatanisha katika toleo lijalo au tuandikie kupitia 0753825794 au barua pepe [email protected]. Tembelea www.hubofwisdom.com/media kufahamu zaidi kuhusu program zetu na kuwa sehemu ya jamii hii. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/hubofwisdom/message
Nov 15, 2023
4 min
KWANINI MAHUSIANO MENGI YA KIMAPENZI HAYADUMU? - Sarah Ngonyani
Kwa uwazi na utaalamu Mis Sarah anaelezea namna ya kudumisha mahusiano ya kimapenzi. Sikiliza --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/hubofwisdom/message
Nov 3, 2023
36 min
WATU
"The more hands you shake, the more opportunities you create." Katika hatua za awali za kujenga biashara au asasi uwezekano mkubwa ni kwamba watakaojihusisha na wewe ni watu wanaokufahamu. Vivyo hivyo ili watu wakufungulie milango ya fursa kigezo kimoja wapo kikubwa ni namna gani wanakufahamu. Fuatilia mtiririko wa episode hizi katika YouTube: H.W TV na Podcast: H.W PODCAST kila wiki. Maoni yako ni muhimu na atunayathamini sana, hivyo tuma ujumbe wako wa sauti kwa njia ya WhatsApp nasi tutaumbatanisha katika toleo lijalo au tuandikie kupitia 0753825794 au barua pepe [email protected]. Tembelea www.hubofwisdom.com/media kufahamu zaidi kuhusu program zetu na kuwa sehemu ya jamii hii. Tunapenda sana ukisikiliza, lakini tunapenda zaidi ukifanya. Kwahiyo fanya zaidi na uwe zaidi. Cheers! --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/hubofwisdom/message
Oct 30, 2023
5 min
MIPANGO
Watu wengi hudhani kuwa wakipata fedha nyingi ndio watafanya mambo fulani makubwa. Lakini ukweli ni kwamba wengi hawana umadhubuti wa matarajio yao, yapo hewani tu. Fuatilia mtiririko wa episode hizi kwa katika YouTube: H.W TV na Podcast: H.W PODCAST kila wiki. Maoni yako ni muhimu na atunayathamini sana, hivyo tuma ujumbe wako wa sauti kwa njia ya WhatsApp nasi tutaumbatanisha katika toleo lijalo au tuandikie kupitia 0753825794 au barua pepe [email protected]. Tembelea www.hubofwisdom.com/media kufahamu zaidi kuhusu program zetu na kuwa sehemu ya jamii hii. Tunapenda sana ukisikiliza, lakini tunapenda zaidi ukifanya. Kwahiyo fanya zaidi na uwe zaidi. Cheers! --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/hubofwisdom/message
Oct 25, 2023
1 min
SIRI ZA USHINIDI - Halima Kopwe (MISS WORD TZ 2023)
'From a Rough to a Diamond' Mis. Halima Kopwe anaelezea safari yake ya ushindi na kile anachowashauri vijana wengine wenye kiu ya kustawi katika nyanja walizopo. EDITION 4 - THE WISE MEGA MEET-UP (Episode) Tembelea www.hubofwisdom/media kuangalia na kusikiliza zaidi. Toa maoni yako ili jukwaa hili lizidi kuwa bora kwa ajili yako, tumia 0753825794 au tuandikie katika barua pepe [email protected] Welcome at the home of positive vibes! #karibu_nyumbani --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/hubofwisdom/message
Oct 25, 2023
6 min
DONDOO ZA MPENYO WA KIUCHUMI - James Mwang'amba.
"Tunaposema mpenyo wa kifedha maana yake ni kwamba mtu anatoka sehemu moja ya chini na kwenda katika sehemu nyingine ya juu. Ushindani ni mkubwa na hakuna mtu anayejali kwamba unalia au unalalamika. Watu wanataka kuona kwamba unaleta nini mezani." Anasema James Mwang'amba. Fuatilia muhtasari huu wa mazungumzo ili kufahamu dondoo za kukuweka sehemu ya juu kifedha katika eneo lako la kazi au biashara na maisha binafsi. Toa maoni yako kupitia www.hwtz.wordpress.com au tutumie ujumbe wako wa sauti na tutauambatanisha katika toleo lijalo. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/hubofwisdom/message
May 3, 2023
19 min
MALENGO (Goal Setting) - Anthony Luvanda
Unachotakiwa kufahamu kuhusu malengo. Anthony Luvanda anazungumzia manufaa ya kuweka malengo, sababu zinazowafanya watu wengi wasizingatie kuweka malengo na Kwanini watu wengi wenye malengo wanashindwa kutekeleza. Ufanye mini kuliepuka hilo? Tia maono yako kuhusu toleo hili. Tuma ujumbe wa sauti na kuelezea ulichojifunza nasi tutaambatanisha katika toleo lijalo. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/hubofwisdom/message
Feb 28, 2023
38 min
Load more