
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Vijana huko visiwani Zanzibar nchini Tanzania, mashariki mwa bara la Afrika wameshiriki mafunzo ya kuimarisha amani na kuchochea maendeleo endelevu miongoni mwa wanajamii.Halikadhalika Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP nchini humo kwa kushirikiana na wadau wengine wengine wa maendeleo pia yalijikita katika kuwajengea vijana hao uelewa kuhusu Afya ya Akili, usaidizi wa kisaikolojia na kijamii. Rashid Malekela wa UNDP Tanzania amehudhuria mafunzo hayo na kutuandalia mada hii kwa kina, kuelekee visiwani Zanzibar kumsikiliza Pia tunakuleteamuhtasari wa habari:Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya Uhamiaji (IOM) na Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) yametoa wito wa kuongeza msaada wa kibinadamu nchini Sudan, ambako watu milioni 15.4 wanahitaji huduma za dharura za malazi, huku uhaba wa fedha ukipunguza uwezo wa kuwasaidia. Mkuu wa Ujumbe wa IOM nchini Sudan, Mohamed Refaat, amesema akiba ya misaada inaelekea kuisha. “Jana tu, tulikuwa na malori 16 yaliyowasili Darfur, lakini hayo ndiyo yalikuwa ya mwisho katika akiba yetu. Tunakabiliwa na matatizo makubwa.Sasa afya, Chanjo mbili mpya zinazofanyiwa utafiti dhidi ya Ebola zitaongezwa katika majaribio ya kitabibu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wakati nchi hiyo ikikabiliana na mlipuko wa virusi vya Bundibugyo.Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amezitaka nchi duniani kuheshimu sheria za kimataifa na kuepuka matumizi haramu ya nguvu, akionya kuwa migogoro, ukosefu wa usawa na mabadiliko ya tabianchi vinatishia ushirikiano wa kimataifa. Akizungumza leo katika Chuo Kikuu cha Salamanca nchini Hispania, Guterres ametaja migogoro ya Ukraine, Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Gaza na Yemen, akisisitiza umuhimu wa diplomasia na ulinzi wa raia. Ameonya pia kuwa matumizi ya fedha nyingi za kijeshi huku misaada ya kibinadamu na maendeleo ikipungua yanaongeza changamoto duniani.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Nov 6
10 min

Matumizi ya pombe, ukatili wa kijinsia na migogoro ya kijamii ni miongoni mwa changamoto zinazokwamisha amani katika baadhi ya maeneo nchini Uganda. Hata hivyo, wanawake wamekuwa mstari wa mbele kutafuta suluhu, huku zaidi ya wapatanishi 1,500 wakipatiwa mafunzo ya kuzuia migogoro na shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Wanawake UN Women kabla haijaongezeka. Augustine Aramba na taarifa zaidi.
Nov 5
2 min

Mashambulizi dhidi ya mifumo ya maji katika maeneo yenye migogoro yameongezeka mara tatu kati ya mwaka 2021 na 2025, yakihatarisha maisha ya mamilioni ya watu, hususan watoto. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, linasema hali hiyo inawaweka watoto katika hatari ya magonjwa, utapiamlo na ukatili. Flora Nducha ameisoma ripoti hiyo na anatupa maelezo zaidi.
Nov 5
3 min

Hii leo jaridani tunaangazia athari za vita kwa upatikanaji wa maji, Siku ya Kimtaifa ya Kukuza Uelewa Kuhusu Tsunami, na Juhud iza wanawake nchini Uganda za kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa amani.. Mashambulizi dhidi ya mifumo ya maji katika maeneo yenye migogoro yameongezeka mara tatu kati ya mwaka 2021 na 2025, yakihatarisha maisha ya mamilioni ya watu, hususan watoto. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, linasema hali hiyo inawaweka watoto katika hatari ya magonjwa, utapiamlo na ukatili.Hii leo ni Siku ya Kimtaifa ya Kukuza Uelewa Kuhusu Tsunami. Binafsi kwa ufupi ninaweza kukweleza kuwa Tsunami ni msururu wa mawimbi makubwa yanayotokana na mtikisiko wa maji chini ya Bahari lakini Kamal Kishore, Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kupunguza Hatari za Maafa ambaye pia ni Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupunguza Hatari za Maafa au majanga (UNDRR) katika kuadhimisha siku hii, ameeleza hatua tatu muhimu ambazo ukizichukua zinaweza kukuokoa dhidi ya tsunami. Anold Kayanda anatusaidia kueleza kwa lugha ya KiswahiliMatumizi ya pombe, ukatili wa kijinsia na migogoro ya kijamii ni miongoni mwa changamoto zinazokwamisha amani katika baadhi ya maeneo nchini Uganda. Hata hivyo, wanawake wamekuwa mstari wa mbele kutafuta suluhu, huku zaidi ya wapatanishi 1,500 wakipatiwa mafunzo ya kuzuia migogoro na shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Wanawake UN Women kabla haijaongezeka.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Nov 5
9 min

Kama nilivyokudokeza hapo awali, hii leo ni Siku ya Kimtaifa ya Kukuza Uelewa Kuhusu Tsunami. Binafsi kwa ufupi ninaweza kukweleza kuwa Tsunami ni msururu wa mawimbi makubwa yanayotokana na mtikisiko wa maji chini ya Bahari lakini Kamal Kishore, Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kupunguza Hatari za Maafa ambaye pia ni Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupunguza Hatari za Maafa au majanga (UNDRR) katika kuadhimisha siku hii, ameeleza hatua tatu muhimu ambazo ukizichukua zinaweza kukuokoa dhidi ya tsunami. Anold Kayanda anatusaidia kueleza kwa lugha ya Kiswahili.
Nov 5
2 min

Zipporah Achieng, mama kijana nchini Kenya, ambaye aliwahi kuhofia kuhukumiwa alipokwenda kliniki kupata huduma za afya baada ya kujifungua, sasa amegeuka kuwa mhamasishaji wa afya ya uzazi kwa vijana. Kupitia mpango wa Together for SRHR, unaotekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika manne ya Umoja wa Mataifa kwa lengo hilo la kuelimisha vijana na vijana balehe kuhusu afya ya uzazi, Zipporah anawasaidia vijana kupata taarifa sahihi na huduma za afya ya uzazi bila unyanyapaa. Augustine Aramba na taarifa zaidi.
Nov 4
2 min

Hali ya kibinadamu nchini Sudan inazidi kuwa tete huku mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (droni) yakilenga miundombinu muhimu ya kiraia, ikiwemo vituo vya nishati na mafuta, kuvuruga huduma za afya na maji na kuweka hatarini maisha ya maelfu kwa maelfu ya raia. Flora Nducha anatujuza zaidi
Nov 4
2 min

Hii leo jaridani tunaangazia hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda afya ya binadamu, hali ya kibinadamu nchini Sudan, na juhudi za wahamasishaji na mashirika ya UN za kuhusu huduma za afya ya uzazi kwa vijana nchini Kenya. Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) inasema hatua sita zinazoweza kuchukuliwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda afya ya binadamu zina uwezo wa kuokoa maisha ya watu milioni 1.6 kila mwaka, huku zikizalisha manufaa ya kiuchumi yenye thamani ya matrilioni ya dola.Hali ya kibinadamu nchini Sudan inazidi kuwa tete huku mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (droni) yakilenga miundombinu muhimu ya kiraia, ikiwemo vituo vya nishati na mafuta, kuvuruga huduma za afya na maji na kuweka hatarini maisha ya maelfu kwa maelfu ya raia.Zipporah Achieng, mama kijana nchini Kenya, ambaye aliwahi kuhofia kuhukumiwa alipokwenda kliniki kupata huduma za afya baada ya kujifungua, sasa amegeuka kuwa mhamasishaji wa afya ya uzazi kwa vijana. Kupitia mpango wa Together for SRHR, unaotekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika manne ya Umoja wa Mataifa kwa lengo hilo la kuelimisha vijana na vijana balehe kuhusu afya ya uzazi, Zipporah anawasaidia vijana kupata taarifa sahihi na huduma za afya ya uzazi bila unyanyapaa.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Nov 4
9 min

Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) inasema hatua sita zinazoweza kuchukuliwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda afya ya binadamu zina uwezo wa kuokoa maisha ya watu milioni 1.6 kila mwaka, huku zikizalisha manufaa ya kiuchumi yenye thamani ya matrilioni ya dola. Anold Kayanda ameifuatilia ripoti hiyo na kuandaa taarifa ifuatayo.
Nov 4
2 min

Wakazi wa Lui, jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini wanalilia amani, elimu na fursa za ajira kwa vijana baada ya kuchoshwa na vita. Kilio hicho kimetolewa wakati walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS, walipotembelea eneo hilo kusikiliza changamoto za wananchi kupitia kampeni ya Hear Us, Act Now for Peace yaani Tusikilize, Chukua Hatua sasa kwa ajili ya amani. Cynthia Akhangwa na taarifa zaidi.
Nov 3
2 min
Load more